Karibu Sana katika Blogu hii ambayo inakupa fursa ya kupata habari mbali mbali za maswala ya urembo nk. pia kama unatangazo lako unataka liwekwe hapa mtandaoni,usisite kuwasiliana nasi kwa mawasiliano haya +255786665555 au email hii flauwo@yahoo.com.
Monday, December 5, 2011



Hawa ni baadhi ya wavuvi haramu wakinyoosha mikono juu ikiwa ni ishara ya kujisalimisha baada ya kukamatwa na Askari wanaofanya doria pamoja na kupambana na uvuvi haramu katika ziwa Vivtoria


Wahenga walisema za mwizi ni Arobaini lakini pongezi kwa serikali ya Tanzania pamoja na Taasisi zote zinazofanya jitihada mbadala kuweza kupambana na uharibifu huu wa Ziwa Victoria na kufanikiwa kuwakamata watu kama hawa kabla ya Arobaini yenyewe kwa sababu ingesubiria mpaka Arobaini yenyewe basi hata uharibifu ungezidi na kuharibu kabisa uhalisia wa ziwa Victoria na kubakia tu historia kitu ambacho ni hatari kwa vizazi vijavyo


Ziwa victoria linasifika kwa kupatikana kwa samaki aina ya Sangara pamoja na Sato nakuweza kuinufaisha tanzania kiuchumi ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa Vijana wengi nchini Tanzania halikadhalika nje ya Tanzania hususani nchi zinazozungukwa na ziwa hili ikiwemo nchi zote za Afrika Mashariki

Ziwa Victoria pia ni tegemezi kwa Shughuli mbalimbali za usafirishaji wa mizigo pamoja naAbiria katika nchi Zote zinazozungukwa na ziwa hili .




 
© FLORAH | 1:45 PM | Permalink |


Idadi Ya Maoni: 0


Idadi ya watu