Karibu Sana katika Blogu hii ambayo inakupa fursa ya kupata habari mbali mbali za maswala ya urembo nk. pia kama unatangazo lako unataka liwekwe hapa mtandaoni,usisite kuwasiliana nasi kwa mawasiliano haya +255786665555 au email hii flauwo@yahoo.com.
Wednesday, December 14, 2011




















































































































































































































































































































Hii ni hali halisi katika mkutano wa hadhara uliofanyw na mbunge wa Nyamagana Mhe.Ezekieli Wenje katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Nsumba

Mbunge Huyo alikuwa akizungumza na wakazi katika jimbo la Nyamagana na kuweza kusisitizia mambo muhimu katika elimu pamoja na mchakato wa uundwaji wa katiba mpya

katika kuhakikisha tatizo la miundo mbinu katiaka shule za sekondari pamoja na msingi Mhe.Wenje ameahidi kufikia January 2013 tatizo hilo litakuwa limemalizika

Amesema kupitia mfuko wa kuendeleza Elimu katika jimbo la Nyamagana maarufu kama NYAMAGANA EDUCATION FOUNDATION iliyosajiliwa mwaka huyo na kufanya harambe ambayo waliweza kupata shilingi milioni 49 wakati wauzinduzi lakini lengo kuu lilikuwa ni kupata milioni mia mbili watahakikisha kuwa tatizo la mindo mbinu linamalizika

Pamoja na hayo Mhe.Wenje amesema pamoja na kufanikiwa kupata kiasi hicho cha pesa bad wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja wafanyabiashara wanaogopa kuchangia katika Harambe zao kwa sababu wanaogopa kufilisiwa na sreikali ya chama cha mapinduzi lakini ametaja changangamoto nyingine ni pamoja na matajiri wengi kutokupeleka watoto wao shule za hizi za kata lakini akaahidi kushulikia tatizo hilo kwa kuhakikisha anatafuta mbinu mmbala

Pamoja na changamoto hizo Mhe.Wenje ametaja mafanikio waliopata ni pamoja na kuweza kutengeneza madawati 500,Kati ya madawati hayo madawati 400 ni kwa ajili ya shule za sekondari na madawati 100 kwa ajili ya shule za Msingi .Madawati hayo yameweza kupunguza tatizo hilo kwani madawati hayo yanauwezo wa kuhudumia zaidi ya wanafunzi 800

Mbali na maswala ya Elimu pia mbunge huyo akaweza kuzungumzia suala la katiba na kusema woa kama cha cha Demokrasia na maendeleo watahakikisha katiba mpya lazima inakuwa na masilahi kwa wananchi na ndio maana wabunge wa CHADEMA wameweza kupinga mswada wa katiba kwa sababu kuu mbili ikiwa ni pamoja kupinga kwa wananchi kutoshirikishwa vya kutosha ikiwa ni pamoja na kutoa maoni yao juu ya undwaji wa katiba hiyo,

Pili ni kuwepo na vipengele kadhaa ambavyo haviko wazi ikiwa ni pamoja na kumpa Rais mamlaka makubwa .Pamoja na hayo mbunge huyo akaweza kutoa baadhi ya mapendekezo kadhaa kama walivyoadhimia katika chama kama vile kushauri kuwepo na wajumbe wawilwawili kutoka katika taasisi mbalimbali kama vile kutoka katika vyama vya siasa,vyma vya wafanya kazi,taasisi za dini n.k

Pamoja nakusema hayo yote mbunge huyo ameweza kuwashukuru wananchi wa Nyamagana na kuahidi kutatua kero zao ikiwa ni kuzingatia maoni,ushauri pamoja na maswali aliyoulizwa na wananchi wa jimbo la Nyamagana

































 
© FLORAH | 8:03 PM | Permalink |


Idadi Ya Maoni: 0


Idadi ya watu