Karibu Sana katika Blogu hii ambayo inakupa fursa ya kupata habari mbali mbali za maswala ya urembo nk. pia kama unatangazo lako unataka liwekwe hapa mtandaoni,usisite kuwasiliana nasi kwa mawasiliano haya +255786665555 au email hii flauwo@yahoo.com.
Saturday, December 3, 2011



Pamoja na serikali kuhakiki inapanga mipango dhabiti kupambana na magugu maji katika ziwa victoria bado hali inaonekana kuwa tete baada ya magugu maji hayo kuzidi na kusababisha hali yak utofahamu nini mipago endelevu juu ya upambanaji na magugu maji hayo

Ziwa victoria ni moingini mwa maziwa makubwa duniani na hutegemewa na wakaazi wa jiji la mwanza kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile uvuvi wa samaki aina ya sangara pamoja na Sato

Pia ziwa victoria hutumika na nchi za Afrika mashariki katika nyanja ya usafirishaji mizigo pamoja na Abiria lakini kuwepo kwa magugu maji hayo ambayo kuna sababisha hata kina cha maji pamoja na upana wa ziwa hili maarufu na tegemezi katika kukuuza uchumi wa nchi kwa ujumla kupungua siku hadi siku

Licha ya magugumaji hayo kuonekana tatizo katika ziwa Victoria pia hata shughuli nyingine za kibinadamu kumesababisha uharibifu mkubwa shughuli hizo ni kama vile kuoga ziwani kulima mbogamboga kando ya ziwa pamoja na kutiririsha maji machafu ambayo hutumika kuoshea magari maarufu kama car wash


 
© FLORAH | 2:46 PM | Permalink |


Idadi Ya Maoni: 0


Idadi ya watu