Karibu Sana katika Blogu hii ambayo inakupa fursa ya kupata habari mbali mbali za maswala ya urembo nk. pia kama unatangazo lako unataka liwekwe hapa mtandaoni,usisite kuwasiliana nasi kwa mawasiliano haya +255786665555 au email hii flauwo@yahoo.com.
Thursday, November 24, 2011




Huyu ni mwaandaji wa warsha ya kupambana na ukatili dhidi ya maalibino maarufu kama "under the same sun" Vicky Mtetema akifanya mahojiano na waandishi wahabari baada ya warsha hiyo na kuiomba serikali kufuatilia pamoja na kutoa hukumu kwa wale waliohusika na mauaji ya albino ili kuweza kutokomeza kabisa vitendo hivyo viovu.Pia vicky hakusita kuishangaa serikali pale aliposema serikali imeunda kikosi kazi ili kupambana na maauji haya ya maalibino ili hali kikosi kazi cha kwanza hakijaweza kuwasilisha taarifa yake ya uchunguzi na kuiomba serikali kuangalia hili kwa kina ili kuweza kubaini wale wanaojihusisha na mauaji haya ikiwa ni pamoja na kupitia upya leseni za waganga wajadi ambao kwa asilimia kubwa wao ndo chanjo cha unyama huyu

Vicky alisema kuwa waganga wajadi huwadangaja wateja wao kuwa viungo vya alibino huweza kuwafanya waweze kupata wanachokihitaji ikiwa ni pamoja na kufanikiwa katika biashara n.k .Hivyo humlazimu mteja huyo kufanya mbino yoyote ili kuweza kupata viungo hivyo.



Pia Vicky hakusita kuipongeza serikali kwa juhudi ambazo imezifanya kuweza kupunguza mauji haya ya ngugu zetu Alibino



 
© FLORAH | 9:44 AM | Permalink |


Idadi Ya Maoni: 0


Idadi ya watu