Karibu Sana katika Blogu hii ambayo inakupa fursa ya kupata habari mbali mbali za maswala ya urembo nk. pia kama unatangazo lako unataka liwekwe hapa mtandaoni,usisite kuwasiliana nasi kwa mawasiliano haya +255786665555 au email hii flauwo@yahoo.com.
Thursday, March 31, 2011
SAFARI YANGU YA LOLIONDO KWA BABU WA KKKT KUNYWA,KIKOMBE,KIMOJA,TUUUUUU!!!! NDIO WAMEANZA KULIPA JINA LA KKKT,TWENDE PAMOJA NIKUMBEEE!!

Tulitoka mwanza siku ya jumatano ya tar, 23/3/2011 asubuhi ya saa nne tulipita njia ya NDABAKA Tukaanza kukata pori la Serengeti,tulipita kwenye mto wa viboko unaoitwa HIPPO POOL. TWENDE SASA!!!!
Hao ni viboko wametulia ndani ya maji tope.
TWENDE SASA!!
Soma mwenyewe!! hicho kibao kipo hapo jirani ya mto

Shost barabara mvua ikinyesha ni balaa tupu.tulikuta majuzi yake magari yalicheza rumba ya kutosha hapa TWENDE SASA!!
Kipenzi changu Conso yulikuwa pamoja baridi ilitutandika kisawasawa
Hatimae tulifika Wasso Loliondo. Nilivyoona hiki kibao kimeandikwa LOLIONDO NILIPATA MATUMAINI KUWA TUMEFIKA,SHOST SIKUJUA KAMA NDIO KWAAAANZA SAFARI IMEANZA


Tulisogea kama kilomita 65 hivi tukakutana na foleni ya kanda ya ziwa,Shost hapa bado hatujazikuta gari za Arusha, Hapa tulilala mpaka morning bila kusogea.TWENDE SASA!
Asubuhi tulisogea kiduuuuuchu!! tukawa makutano ya arusha na kanda ya ziwa,Hapa sasa ndio usiseme mbuzi anauzwa laki 250,000 na akichinjwa kabla hajachunwa ngozi ameisha,wa mguu,kichwa,mbavu,utumbo shost hadi miguu inagombaniwa,
Njiani tulikutana na gari kibaaao zimeharibika na wenye nazo wamezitelekeza kwa uchovu.
Kule hakuna cha mdosi wala mdhungu,gabacholi, machinga kama mimi,maskini yani shost wooote ni foleni.
Shost tulisogea tena baada ya siku mbili tukawa kwenye kijisenta kipo kati hapo, TUKO PAMOJA???????
Hapo tulidodaje!! mtandao ulikuwa tabu wee acha kabisa,hapo machinga nimependa juu ya mti nipate kujua umachinga huko nyuma vipi.
Shost tairi zilikuwa zikijazwa upep0 na ile ya kujazia pikipiki,Upooo?
Hooooooooi! matumaini yanapotea kila dakika shost.
Eee bwana ee! sisi tulienda kisisita duu tukabeba maji na tubiskuti kumbe wenzetu walibeba majiko, ndizi,dagaa,unga,na vikorokoro vyooote kama unavyoona mwenzetu hapo anaandaa lanchi,



SHOST HAPA SASA!!UNAJUA KWA BABU HUTAKIWI KWENDA NA NANIHIII KAMA HIZI KWANI UKIFIKA NAZO KULE NI KIZAZAA KITUPU,HIVYO WENYE NAZO WALIANZA KUZITELEKEZA KWA BARABARA KAMA HIVI. UPO HAPOOO!!!!!!!!!!
Mangi mimi na uroha wa nyamazzzz niliumwaje tumboo!! nahisi nilikula hazijaiva vizuri,Usiulize kilichoendelea hapo shost nilitamani kurudia njiani. na ujue hapo ni siku ya tatu kwa barabara ni kusogea kiduchu na kulala.
Kilichonistaajabisha na kunishangaza ni jinsi maeneo yote barabara nzima ni kinyesi hapa,nyama choma pembeni,mwenye jiko lake kwa jirani hapo hapo,zile ngozi za mbusi na ngombe nazo zimetupwa hapo hapo ILA NZI NDIO HAMNA HATA MMOJA.
Maji sasa wasonjo wa kimasai wanafanya bizineee acha kabisa, hiyo ni chai iko jikoni na hiyo rangi ni ya maji wala sio majani,Na unakunywa tena kwa kugombania,Shost chooonde chonde ukienda ukumbuke kajiko baasi na maji ya kutosha,Ukijidai kujaza watu kwenye gari ujue itakula kwako,acha nafasi ya kuweka misosi.
Nyamazzzz inagombaniwa hapo



WAMASAI WANACHANGANYIKIWA NA CHAPAA WANALEWA HADI NANIHII WANAZISAHAU JUUU
Nimefurahi sana serikali yetu walivyositisha watu kwanda mpaka wafanye utaratibu flani,kwani kwa hali hii mlipuko wa magonjwa ulikuwa wa kufikia.
Mlima wa dawa huo kwa babu kikombe
Kaeni mtulie mkifanya fujo babu anastopisha kikombe.ila kila mtu atapata kikombe.

Baada ya kuchemsha dawa babu anatunza mazingira kwa kuyachoma makapi ya dawa
Babu house
Jamani ambao ndio mnajiandaa kwenda naomba muwapelekee zile kata za kuchotea dawa kwani wanaungua kweli wakati wa kuchota dawa.
Hemazz hizo!kulala elfu kumi tuu kwa kichwa.


Hatimae yulifika kwa babu tukapata kikombe baada ya kuhamua kuiacha gari na kutembea kwa tz 11 kwa miguu zaidi ya kilomita 20 hapo piki piki huwezi kupanda labda uwe umezidiwa na tofauti na hapo getini hupiti.SHOST POLE KWA KUKOSA MATUKIO MENGINE MENGINE KWANI HUKO UKIONEKANA UKIPIGA PICHA NA UGOMVI KWELI SANA.ILA KIUKWELI NILIONA VITU VYA AJABU SANA WATU WANAUMWA SAAAANA NA ZAIDI KUNA NJEMBA MOJA ILIVYOKUNYWA TUU DAWA NYOKA ALICHOMOKA KWANYE SURUALI NA WAMASAI WAKAMUUA NA YEYE AKAFA HAPO HAPO.


KWAHERI SHOST ILA MIMI NIMEPONA PUMU YANGU ILOKUWA INANINYANYASA KIPINDI KIREFU SANA.KWANI UKIAGA UNAENDA KWA BABU NI AIBU???? NILIWAKUTA MASHOT WALIONIAGA WANAENDA GUANZUUU WAKIWA KWENYE FOLENI YA KUSUBIRI KUNYWA KIKOMBE KIMOJA TUU CHA BABU
 
© FLORAH | 3:37 PM | Permalink |


Idadi Ya Maoni: 15


  • Tarehe March 31, 2011 5:27 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    dada kumbe na wewe hukuwa nyuma kupata mugariga

     
  • Tarehe March 31, 2011 10:23 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    asante kwa picha hizo na ushuhuda uliotupa kwamba umepona nashukuru mungu umepona dada yangu kampeleka mwanae alipata stroke miaka 4 iliyopita akiwa na miaka 10.kaangaika hospzote namwombea mungu amponye maana mtoto anashindwa kwenda shule mpaka leo hope akirudi mungu atamponya kila la heri.mdau wa texas

     
  • Tarehe April 1, 2011 1:22 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    pole na safari asante kwa matukio ya loliondo kwenye picha. pia naona umeandika kwa watu wanaokwenda wapeleke vya kuchotea dawa mi kwa ushauri wangu wewe kama sadaka yajo ya asante ungewapa watu wanaokwenda wampelekee au peleka kwenye kanisa la kkkt hapo mwanza nadhani watafikisha kwa babu

     
  • Tarehe April 1, 2011 2:35 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Pole sana.Usiwajali hao mashost wako wasiojua kuaga.Mungu ni mwema mshukuru siku zote.

     
  • Tarehe April 1, 2011 1:15 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    aaaaaahaaaaaaa!!! Dada Florah umeniacha hoi, eti watu walikuaga wanaenda China ukawakuta kwa babu. Jamani msione aibu kuaga mnaenda kwa babu sababu babu si mganga wa kienyeji

     
  • Tarehe April 1, 2011 1:35 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    MBONA UNAJISHUKU NA PUMU ...!! SEMA TU UKWELI..!!!. ILA POLE SHOTI KWANI SHUGHULI ILIKUWA KUBWA.

     
  • Tarehe April 1, 2011 9:49 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    SHOST KWANI NANI AMEKUULIZA ULICHOENDEA KWA BABU SANGOMA HUYO?SEMA TUU UKWELI TUKUELEWE MAMA.

     
  • Tarehe April 1, 2011 9:52 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    filo watu wengine wana mijiwivu kweli hao wadau waliopita wana matatizo sana naomba uwasamehe bure. hongera sana kupata kikombe kwani mimi natamani kwenda ila kazi zinanibana sana.ila mamii nimevunjika mbavu kuona eti ulikuta waliokuaga wanaenda guanzuu kwa babu.hawakuona aibuuuuuu!!!!?

     
  • Tarehe April 2, 2011 2:06 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Umenichekesha sana, kuwakuta watu ambao walificha siri kuwa wanaenda kwa babu!! Hivi duka lako liko wapi? Nitakuja Mwanza likizo? Ningependa kupitia tujuane! Blog yako inatusaidia kujua mengi sisi wa nje ya nchi.

     
  • Tarehe April 3, 2011 1:51 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    SAFIIII SAAAAAANA!!WENYE MIJIWIVU JINYONGENI TUU!! HONGERA SANA MAMA NA MIMI NIMEPONA TAKA TAKA ZOOOOOTE ZILIZOKUWA MWILINI MWANGU.HATA KAMA HUMWAMINI BABU HUPASWI KUMWITA SANGOMA ATI!

     
  • Tarehe April 3, 2011 1:51 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    SAFIIII SAAAAAANA!!WENYE MIJIWIVU JINYONGENI TUU!! HONGERA SANA MAMA NA MIMI NIMEPONA TAKA TAKA ZOOOOOTE ZILIZOKUWA MWILINI MWANGU.HATA KAMA HUMWAMINI BABU HUPASWI KUMWITA SANGOMA ATI!

     
  • Tarehe April 4, 2011 6:06 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Dear asante sana kwa kutupatia hali halisi ya Loliondo.Hayo manyang'au mawili yaliyotangulia nafikiri ni yale yaliyokuaga yanaenda Londan ukayakuta Loliondo looh, aibuuuuuu.Kwani kwenda Loliond ni nini? Mawivu tuu yatabakia kulalama.Yanatakiwa yavue hayo makatambuga yao kama yanataka kufanikiwa kimaisha kama wewe.Kiatu cha wivu... kivueeeee..

     
  • Tarehe April 5, 2011 4:11 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    safi umefanya jambo la maana kutuonyesha mazingira maana wengine hata hatujui pakoje!pole na heka heka za huko!nakutakia kila la heri kama imekusaidai

     
  • Tarehe April 5, 2011 10:16 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Ikiwezekana Mjengwa, mashaka, na Mwilima watembelee blog yako ili wajifunze mambo.

    Nakupongeza sana dada Flora kwa picha na ushuhuda wako.Niko nje ya nchi natamani sana na mimi ningepata kikombe cha babu kinipunguzie adha ya magonjwa ya mwilini.Nimepima hapa miaka 7 yote sipati ugonjwa lakini nasikia maumivu mwilini na nafanya kazi vema wala sijawahi kulazwa.

     
  • Tarehe April 6, 2011 11:50 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Hongera sana dada filo kwa kutuwekea habari za lolindo,kweli kabisa nakupongeza kwa hili kwani tumezoea kuona tuu picha za viongozi wakibugia dawa na babu akiongea kuhusu dawa, ila kiukweli tulikuwa hatujapata story kamaili ya njia nzima, vituko kama hivyo,, na mazingira yalivyo.NAMUUNGA MKONO MDAU ALIEPITA.

     
Idadi ya watu