Karibu Sana katika Blogu hii ambayo inakupa fursa ya kupata habari mbali mbali za maswala ya urembo nk. pia kama unatangazo lako unataka liwekwe hapa mtandaoni,usisite kuwasiliana nasi kwa mawasiliano haya +255786665555 au email hii flauwo@yahoo.com.
Sunday, March 7, 2010
                              Enyi watu wa mungu tuombeeni huku kanda ya ziwa kwani maovu yanaendelea kutuzidi, mara ujambazi, vifo vya maalbino, mkoa wa mara ndio kabsaa usiseme kwani mbali na kuchinjana kama kuku pia wanaendekeza imani za kishirikina, na ndio kilichompata huyu mtoto magath kwani alikatwa mikono na mtu asiejulikana kwa madai kuwa viganja vyake vina michoro ya utajiri, 


Siku za mwisho itakuwaje? nani atahukumiwa zaidi? ni mganga,au muuaji?
                                        mtoto magatha akiwa hosipitali ya mkoa
                         Pole sana mwanetu mungu atakusaidia, na waliokukata mikono yako ipo siku wataadhibiwa  na kupata mateso kuliko waliyokupa.tushirikiane wote kumwombea.
 
© FLORAH | 9:31 AM | Permalink |


Idadi Ya Maoni: 4


  • Tarehe March 7, 2010 10:52 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Eee mungu mbona umeleta kiama kwa njia kama hizi? watu wa mara wakati wa kubadilika umefika acheni ukatili usiokuwa na maana mwaogopeni mungu

     
  • Tarehe March 8, 2010 12:26 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Inasikitisha sana kuona unyama huu bado unaendela katika hii karne ya 21. Hayo mateso ambayo amepewa huyo malaika hayana kipimo. Na mtu ampaye ametenda hicho kitendo inaonyesha ni mtu wa karibu san na anaye wajua vizuri wazazi wa huyo mtoto. Kitu ninchojiuliza mtu alietenda kitendo hicho hajulikani vipi wemeweza kumjua mtu huyo alikuwa anatafuta kwa madai kuwa viganja vya mtoto vina michoro ya utajiri isipokua mtu alietenda kitendo hicho ndio ametoa siri ya viganja?

     
  • Tarehe March 14, 2010 11:56 AM, Mtoa Maoni: Anonymous JULIETH

    Nimeshikwa na bumbuwazi la ajabu! kwakweli huyu mtoto mdogo wanamuonea wa niniiiii na kumpa athabu kama hii? jamani hana hatia.Utajiri ndio mtu afikie unyama kama huu?Wanafamilia mzidi kumuomba Mungu na yeye atajibu tu!

     
  • Tarehe April 6, 2010 1:47 AM, Mtoa Maoni: Blogger judith

    WE NEED TO KILL WAGANGA WOTE WA KIENYEJI WE DON'T NEED THIS SHIT!!!! I DID NOT WANT TO TAKE ANY POSITION IN THE POLITICS BUT I THINK IT IS TIME FOR ME TO GET READY AND GET IN THE GAME!

     
Idadi ya watu